Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima aliagiza Jeshi la Polisi pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ( TAKUKURU) kumkamata na kumhoji mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya Uviko 19
Dk Gwajima alitoa agizo hilo Jumanne Agosti 17, 2021 katika kijiji cha Kyatunge wilayani Butiama akibainisha kuwa Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo linaloivuruga wizara yake na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu.

0 Maoni
TRUE