CHIMBUKO LANGU.
      Naitwa Penius Patrick kutoka Bukoba. kwa ufupi sana nilizaliwa mtoto wa pili katika familia yetu. maisha yangu yote nilitamani sana kuwa Director wa Video. Akili yangu yote iliwazia hicho kitu kila kukicha. Mungu si mbaguzi kwa mwanadamu niliendelea kuwa na maarifa kibao juu ya ndoto hiyo. Nilikutana na watu wengi akiwemo Director Adam Israel
kutoka Dar es salaam ambaye aliamua kunipa ujuzi zaidi wa kuhariri video na jinsi ya kuongoza hizo video wakati wa tukio. 
Baada ya muda mfupi nilipata video ya msanii Lihamond ambayo video hiyo nilipewa kama mtihani. kwa kuwa hii ni ndoto yangu kutoka moyoni haikuwa vigumu kuelewa. Basi baada ya kuhariri video ya Lihamond walioiona hawakutegemea kitu hicho kutoka kwangu.



      katika hiyo video nilipata kumfahamu Director Hanscanna ambaye kwa kiasi kikubwa alinitia sana moyo kwa jinsi alivyonipa historia yake mpaka kuwa Director mkubwa Tanzania na Dunia kwa ujumla. Leo, kesho na kesho kutwa nitakuwa Director mkubwa kwani njia yangu ya kupita nimeshaijua.

SIRI YA MAFANIKIO YANGU MPAKA SASA.
     #KUJITOA
     Mambo yote niliyokuwa nikifanya na ninayoendelea kufanya na watu mbalimbali, ni kwa kujitolea. Sikupenda kutanguliza pesa kwani dhumuni langu kuu ni kutafuta kwanza madini ya uhakika yaani elimu ya maisha kuhusu ndoto yangu. Nawe msomaji wekeza kwanza kujitolea naamini kila kitu kitakuwa sawa maana kuna nguvu kubwa katika kujitolea.

    #UAMINIFU
    Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa moyo wa uaminifu alonipatia. Uaminifu huu kwangu umekuwa zaidi ya pesa. Uaminifu huu umenifanya kuwa mwenye kuaminika kwa watu wakubwa ambao wamekuwa wakinitumia katika shughuli zao mbalimbali. Kuna msemo usemao,
nanukuu, "UAMINIFU NI MTAJI" Hakika ukiwa mwaminifu utaweza kufika mbali kirahisi. Kila ninachofanya hata kama si changu na hata kama hakiniletei manufaa yoyote, lazima nikifanye kwa ufanisi na kwa wakati. 
     
     ELIMU YANGU.

      Watu wengi ninaokutana nao sehemu mbalimbali huwa hawaamini kile ninachowambia kuhusu elimu yangu. wengi hudhani kuwa nimesomea uandishi wa habari au IT. Si kweli kabisa, mimi nimesomea Business Administration katika chuo kikuu cha Ardhi, Dar es salaam, Tanzania. Kulingana na hatua nilizozichukua mwanzo kutafuta ujuzi wa ziada kwa watu, nimejikuta nafahamu mambo mapya ambayo hata sijaenda shule kuyasomea. Ujuzi wa kompyuta na mambo ya mitandao sijasomea bali ni ujuzi nilioupata kwa watu nilioishi nao vizuri. ukiwa kijana lazima ubongo wako na akili zako ziwe na utamaduni wa kutotanguliza pesa ili uweze kufanya kazi vizuri bali utengeneze kwanza mtaji ambao ni jina na Uaminifu.



ZIFUATAZO NI FANI ZANGU KWA UJUMLA.
Video Director 
      Graphic Designer 
Photographer 
Web Designer 
               Computer Technician  

KWA KIFUPI HIYO NDIYO HISTORIA YANGU.
Asante kwa kuwa mmoja wa wale wanaonifahamu.
Tel: +255627498366
       +255747156727
Byebye!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!