BONDIA Twaha Kassim Rubaha ‘Twaha Kiduku’ ameendeleza ubabe kwa rafiki yake, Abdallah Shaaban Pazi ‘Dullah Mbabe’ baada ya kumshinda kwa pointi usiku huu ukumbi wa Ubungo Plazza Jijini Dar es Salaam.
Kiduku alianza vibaya pambano hilo baada ya kuangushwa raundi ya kwanza tu.
Kutoka hapo Kiduku alitawala pambano kwa raundi zote tisa zilizofuatia na majaji wote wakampa ushindi wa pointi 98-91. Pamoja na malipo ya kawaida lakini Kiduku amekabidhiwa gari aina ya Toyota Crown Athlete. Hilo lilikuwa pambano la tatu baina yao kufuatia kutoka droo Oktoba 21, mwaka 2017 ukumbi wa Msasani Club kabla ya Kiduku kushinda kwa pointi Agosti 28, mwaka jana Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

0 Maoni
TRUE