Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Azaria (Dereva), Joel Mitondwa, Said Budi, Bernard Mushingi na Vahadi Hassan wamefariki kwa ajali ya gari katika eneo la Hanseketwa Old Viwawa Wilayani Mbozi Mkoani Songwe leo asubuhi tarehe 23-08-2021.

Wafanyakazi hao ni kikosi kazi cha Fast Track na wamefariki wakiwa wanafukuzana na gari walilokua wanadhani limebeba bidhaa za magendo (halipo kwenye picha), Kamanda wa Polisi Mkoani Songwe, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.