FAHAMU KUHUSU SIKU YA WAPENDA NAO (VALENTINE DAY).

Sikukuu ya wapenda nao maalufu kama Valentine Day  ni siku ambayo ilianzishwa ikiwa na dhumuni la kuwakutanisha wanaopendana ili waweze kujumuika kwa pamoja na kufurahi, wanaweza kuwa ndugu, majirani, wapenzi walioko kwenye mahusiano na wapenzi waliopo kwenye ndoa. Siku hii ilianzishwa miaka 45 iliyopita katika mji maalufu duniani New York nchini Marekani.

                Baada ya miaka 12 badae ilisambaa na kuyafikia mabara yote Duniani na kuifanya kuwa kama sikukuu nyingine maalufu duniani mfano X-Mass, mwaka mpya n.k. Cha kushangaza zaidi mpaka kufikia mnamo mwaka 2002 sikukuu ya wapendanao ilianza kuwatenga watu waliokusudiwa kwenye sikukuu hii na kujikuta wanaosherehekea siku hii ni wale wenye mahusiano ya kimapenzi. Ni mara chache sana kuwakuta ndugu au majirani wakiburudika na siku hii.

                Na usichokifahamu kuhusu sikukuu hii ni kwamba ni sherehe namba tatu duniani inayowafanya walengwa kutumia kiasi kikubwa cha pesa kugharamikia mambo kama mavazi, chakula na mengine yanayoambatana na sherehe hii. Tathimini zinaonesha kuwa sherehe ya kwanza kutumia kiasi kikubwa cha pesa ni Christmass (X-Mass) ikifuatiwa na New Year (Mwaka Mpya) ikishika namba mbili na kufuatiwa na Sikukuu ya wapenda nao (Valentine Day).

                Jambo la kushangaza ni kwamba ijapokuwa sikukuu hii ni ya kimataifa nikiwa na maana kuwa inasherehekewa na nchi zote duniani, ila haina mapumziko ya kikazi, namaanisha shughuli za Kiserikali kote duniani huendelea kama kawaida. Hiyo ndiyo historia fupi ya Valentine Day.

MWISHO KABISA NAKUTAKIA SIKU NJEMA YA UMPENDAE.